
Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS
kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema
kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa anatamani kuwa na msanii huyo kama
mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa ndoto yake hiyo haijaweza
kukamilika mpaka dakika hii.
“Unajua nilikuwa namu admire Wizkid
toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani
wa kiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambaye
nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena
maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli” alisema Linah Sanga.
Katika hatua nyingine msanii huyo kwa
sasa anasema ameamua kufanya tu kazi na kuachana na masuala ya mapenzi
na kusema kuwa akichanganya kazi na mapenzi mwisho wa siku hata kazi
yenyewe anaweza kuharibu.
Linah amedai mpaka sasa ana mipango ya
kufanya kazi na Wizkid ingawa anadai kwa sasa alimwambia yupo ‘busy’
kidogo mpaka siku za usoni ndipo wanaweza kukamilisha kazi hiyo.
Chapisha Maoni