Akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo
kinachorushwa na East Africa Television, Tunda amesema anachukizwa na
kitendo cha watu kujadili mambo yasiyowahusu, pamoja na kuoneana wivu,
na kuwataka wasimfollow kwenye mitandao ya kijamii.
“Wanaonipenda wanipende na wasionipenda
waachane na mimi wasinifollow na kunijazia coments za kipumbavu pumbavu,
ila wanaonipenda wanifollow”, alisema Tunda.
Pia Mlimbwende huyo ambaye ana mahusiano
na msanii wa muziki wa bongo fleva Young Dee, amesema anashangazwa na
tuhuma anazopewa za kutumia madawa ya kulevya, na bado analifanyia
utafiti suala hilo.
“Kitendo cha kuniambia natumia unga mpaka leo sijui limeanzia wapi, hata sijui ila naendelea kufuatilia” alisema Tunda.
Kwa sasa mrembo huyo ameamua kurudi shule baada ya kuacha kwa muda mrefu na kujihusisha na sanaa
Chapisha Maoni