
Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu msanii
mkongwe wa Bongofleva Juma Nature kufunguka kwenye kipindi cha Friday
Night Live (FNL) na kusema kuwa anahitaji shoo moja tu uwanja wa taifa
ambayo itamkutanisha yeye na msanii ambaye kwa sasa anasumbua kwenye
Bongofleva Diamond Platnumz ili kuona nani ni mkali kati yao.
Mashabiki kwenye ukurasa wa Facebook wa
(EATV) walifunguka mambo mengi na wapo watu ambao wanamuunga mkono Juma
Nature wakisema kuwa Diamond Platnumz hatauweza muziki wa Juma Nature
stejini huku wengine wakisema kuwa Juma Nature kwa Diamond Platnumz bado
sana, mvutano wenyewe ulikuwa kama hivi:-
“Diamond ataaibika sana siku akipanda
jukwaani kupambana na Sir Juma Nature, asijekubali suala hilo, maana
yeye (Diamond) hata awe na Dancers wake, Nature akiwa peke yake tu
anatosha kuwaamsha watu, tena uwanja wa taifa pale ndio hata
asithubutu,” aliandika Harrison Haroun Makaye.
“Kujaza uwanja na kushangiliwa na
mashabiki haikusaidii kitu nyanyuka ushindane kimataifa, kweli unajua
kuimba ila tatizo Diamond haimbi muziki kwa kushindana na mtu. Na wala
hajawai kutangaza kuwa yeye ndio anajua kuimba,” hii ni kwa mujibu wa
Phemmy Mkuyawa
“Diamond nyimbo zake ni za kuwaburudisha
na kuwafurahisha masisita du, lakini mzee mzima Juma Nature mistari yake
inasomeka na inakubalika kwa watu wote na rika zote na haina powder
wala nini,” Fine Jerry naye alifunguka hivyo.
“Ha ha ha ha bado haijaniingia hiyo. Juma
Nature na Diamond wapi na wapi? labda angesema tumpambanishe yeye Juma
Nature na wasanii kama kina Chege au Temba hao! ndiyo type yake, ila
King Kiba ndiye apambane na Dangote siyo yeye mimi hilo sijaafikiria
kabisa,” Joyce Jackson aliposti mawazo yake hayo.
“Wajinga wajinga ndiyo watasema Diamond
mkali kuliko Nature msiangalie visenti au video au kaimba na wasanii wa
Nigeria, swali nani mkali kwa kuimba, Diamond mjanja wa kusaka hela na
mishe anaziweza ila kwa kuimba hata Ali Kiba anamzidi. halafu Nature
kuimba ni nature yake sio anaekti,” Rabi Intocavel naye alitupia hiyo.
Hizo ni baadhi ya Comments za watu kutoka
kwenye ukurasa wa Facebook wa (EATV) ambapo mashabiki bado wanaendelea
kuvutana wengine wakisema Juma Nature atamkalisha chini Diamond Platnumz
kama shoo hiyo itakuja kufanyika huku wengine wakisema kuwa Diamond
Platnumz si wa kushindana na Juma Natute wakiwa na maana kuwa lazima
atamshinda Juma Nature.
Chapisha Maoni