Rapper kutokea Manzese Tip Top Connection, Madee amefunguka na kudai
kuwa siku zote atamlaumu msanii wa Bongo flava na aliyewahi kuwa chini
ya usimamizi wa Tip Top, Mb Doggy kwa kuondoka kwenye lebo hiyo.
Akizungumza, Madee amedai Mb Doggy alikosea kuondoka Tip Top kwa kuwa alikuwa chini ya Mikono sahihi.
“Mimi kitu ambacho nitaendelea kumlaumu Mb Doggy ni kuondoka Tip Top,
unajua unapokuwa kwenye malezi ya baba na mama mmoja hata maadili ni
yale yale, unapoenda sehemu nyingine unakutana na vitu vipya, alafu si
tulikuwa tukitoa nyimbo Babu tale ndiyo anaenda kushughulika kila kitu
kupeleka Radio na vitu vingine, sasa hakuwa na Menejimenti kila kitu
alikuwa akifanya yeye baada ya kutoka nahisi ndiyo maana akashindwa”
Alisema.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni