MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum ameamua
kuvunja ukimya kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa msanii huyo wamebwagana
na mama mtoto wake, Zari, kisa mrembo aliyecheza kwenye video mpya ya
Rayvan.
Diamond amejibu tuhuma hizo kwa kumpost Zari kwenye page yake ya
Instagram na kuandika hivi "Roho ya Simba wanajaribu ila hawatokaa
wawezee Nakupenda mpaka Naugua @zarithebosslady Mmmechelewa"Tetesi za
Diamond kutoka na msichana huyo zimekuwa gumzo kubwa instagram
Kauli hii inakuwa mwiba na jibu la kwanza kutoka kwa Diamond baada ya
kuvuma uvumi kuwa amegombana na mama mtoto wake Zarina ‘Zari’ Hassan.
Tetesi zimedumu kwa takribani wiki sasa kwenye mitandao ya kijamii,
ati Icon huyu wa muziki Afrika ya Mashariki ameibanjua amri ya sita na
modo wa kwenye video ya Raymond ‘Kwetu’.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni