0
Kama anavyojiita mwenyewe the king of RNB Bongo na hakuna shaka juu ya hili kwani mwanamuziki Ben Poul anaeiwakilisha kanda ya Kati, ni miongoni kati ya wanamuziki daraja la kwanza wa RNB Tanzania na Afrika mashariki.
Weekend hii star huyu alipigwa na butwaa kuona matangazo kwenye mitandao ya kijamii kuwa, alikuwa na show mjini Singida wakati hata hakuwa na taarifa na hakuwepo katika ardhi hii ya Magufuli.
Ben ameiambia best djs kuwa, alipokea simu nyingi watu wakimuuliza juu ya hilo hali iliyozidi kumuweka njia panda.
“Sasa Rich One nae akanipigia akanambia eti Ben unashow ya Mamiss huku Singida? nikamwambia hapana na wala sikuwepo Bongo, akanambia basi kuna mtu huku kalipwa na PA zinapita anadai yeye ni Ben Poul na ana show huku” Alisema.
Mkali huyu anadai hii ni mara ya tano sasa kujitokeza wakina Ben Poul feki na kutapeli fedha za watu.

Chapisha Maoni

 
Top