0


Rapper Nay wa Mitego kupitia akaunti yake ya instagram amefunguka na kusema kuwa haumizwi kichwa na wasanii wanaomdiss kutokana na staili yake ya muziki.

Nay ameongeza na kusema kuwa hawezi kuwa msanii mkali kama wanavyotaka kwani hao wanaojiita wakali ndio wanaokufa na Njaa.

“Siumizwi kichwa na wasanii wanao ni Diss, nachanganyikiwa nikijua nimepoteza Shabiki wakweli ata Mmoja.!! Sitaki kua Msanii mkali Kama watakavyo wao, Mashabiki wangu wana Enjoy ninachofanya najivunia kuwa na Fans wengi. Wanajisifia Ukali na wanakufa njaa😭😭. #ShikaAdabuYako Imewapa Stress Daaaah #MasterMindScolfild #Team966MoneyMakers #MoneyMusic966” aliandika Nay kama inavyoonekana kwenye picha chini.

Chapisha Maoni

 
Top