Kwa muda mrefu Diva wa muziki wa Bongo
Flava ambaye anajulikana kwa ufundi wake wa kucheza na sauti, Judith
‘Ladyjaydee’ Wambura, alikuwa kimya kikazi (muziki) mpaka hivi juzi
alipoamua kuachia hit inayosumbua vituo kadhaa vya radio nchini ‘Ndi ndi
ndi’.
Star huyu naweza sema amerudi kwa mshindo
mkuu, na hata style aliyoitumia kurejea nayo mimi kama mdau wa muziki
niliielewa sana, nazungumzia ule msemo wa ‘Naamka tena’.
Sasa jana Jaydee akizungumza kupitia
kipindi cha Twenzetu cha Times Fm, ameelezea jinsi alivyopata Idea ya
kutumia msemo huo na jinsi ulivyobamba kitaani.
Jide amedai yeye na timu yake walikaa
kuzungumza ni jinsi gani wanarudi, na katika mawazo yote yaliyowekwa
kujadiliwa mezani ndipo wakakubaliana kutumia ‘Naamka tena’.
“Unajua kuamkaa si lazima uwe ulifumba
macho, atakama ulikaa unaweza sema naamka tena, nilikaa kimya kwa muda
mrefu sasa tukaamua tu hii ije mara moja ‘naamka tena’ nashukuru msemo
ulikuwa mkubwa sana huu” Alisema.
Chapisha Maoni